Wimbo wa chuo

CHUO CHA UALIMU MONDULI

WIMBO WA CHUO

Wimbo: MUNGU WETU KIBARIKI CHUO

  1. Mungu wetu kibariki, Chuo cha Monduli;

    Uongozi na Walimu, wote wabariki.

        :/: Tujalie maisha mema, kazi zetu zibariki;

            Tujalie upendano, ushirika na umoja:/:

 

  1. Utujalie Hekima, Heshima, Adabu;

    Kwa Wakubwa na Wadogo, tusaidiane.

         :/: Tujalie maisha mema, kazi zetu zibariki;

              Tujalie upendano, ushirika na umoja:/:

 

  1. Elimu ni Ukombozi, ni Kauli yetu;

    Tujalie Ufahamu, tunapojifunza.

       :/: Tujalie maisha mema, kazi zetu zibariki;

            Tujalie Upendano, Ushirika na Umoja:/: